29th Graduation Ceremony


TANGAZO LA MAHAFALI

Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania anapenda kuwatangazia Umma wa Watanzania kwamba kutakuwa na mahafali ya 29 kwa wanachuo wote waliomaliza masomo yao katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Kampasi zote (Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Singida, Tanga na Mbeya) kwa muhula wa Septemba 2017 – Juni 2018 mahafali haya yanatarajia kufanyika siku yaIjumaa tarehe 19 Oktoba 2018 katika ukumbi wa kimataifa waJulius Nyerere Dar es Salaam

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora

Kila mhitimu anatakiwa kuzingatia yafuatavyo:-

1. Kuthibitisha ushiriki wake mapema kabla ya tarehe 15 Oktoba 2018 kwa barua au simu zifuatazo:-

Ofisi ya Usajili Kampasi ya Dar es Salaam

ü Simu:022 2123547 – 9 au 022 2131849

ü Simu za Mkononi: 078599231, 0717152111, 0784 321301

ü Whatsapp tu: 0766 795001,

2. Gharama za kukodi skafu ni Shs. 10,000/= (ambayo hairudishwi ikishalipwa)

Malipo ya skafu yafanyike kupitia:Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dar es Salaam, Akaunti namba : 01J1019909100 CRDB BANK .

a)Mazoezi “rehearsal” itafanyika Alhamisi ya tarehe 18 Oktoba 2018 kuanzia saa 2:00 asubuhi kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

b) Majina ya wahitimu yatapatikana katika tovuti ya Chuo: www.tpsc.go.tz kabla ya tarehe 17 Oktoba 2018.

c) Wahitimu wote wanatakiwa kuvaa suti ya rangi nyeusi au “darkblue” na mashati meupe

NYOTE MNAKARIBISHWA